SIMBA leo inacheza na Coastal Union ya Tanga kwenye Uwanja wa
Mkwakwani katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Ni mchezo
unaotarajiwa kuwa mgumu...
Ndugu zangu, salaam za heri nyingi kutoka Unguja,
Tafadhali pokeeni tamko la pamoja la uamuzi wa CUF pamoja na wabunge
wake nchi nzima tulilolitowa leo Machi 18, 2016 baada ya kikao chetu
hapa mjini Zanzibar. Inshallah tusaidiane kuujulisha umma juu ya hili na
dhulma nyingine ambazo mwaziona zikiendelea.
Wasalaam,
Ahmed Nassor Mazrui
Naibu Katibu Mkuu (CUF), Zanzibar
"HAKI SAWA KWA WOTE"
Hatimaye Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ameahidi kuiga mfano wa Rais John
Magufuli, kwenye jitihada za kutokomeza ufisadi nchini mwake, ikiwa ni
pamoja na kusitisha ziara za mawaziri alizozitaja kuwa zinafuja mali za
taifa. Rais Kagame aliyasema hayo mwishoni mwa wiki kwenye mkutano
wa 13 wa faragha wa viongozi wa taasisi zote za serikali nchini humo,
akiahidi kujifunza na kutumia sanaa ya kupunguza matumizi ya fedha za
serikali kama anavyofanya Magufuli. “Ninajifunza kutoka kwa 'tingatinga' la Tanzania, Rais John Pombe Magufuli, lakini nina ushujaa wa kukaza mambo zaidi,” alisema.
Kagame alisema suala la ufisadi nchini humo linachukua mwelekeo mpya na
kasi ya ajabu, na kwamba hawezi kuendelea kulivumilia tena. Akiwa
ameambatana na mkewe mama Jeannette Kagame, kiongozi huyo
alitahadharisha juu ya safari zisizo na tija na matumizi yasiyo ya
lazima ya maofisa wa serikali.